Lewati ke konten utama
Lirik lagu

Moyo Mashine

Ben Pol

Najua kukikucha ntajuta kama nikikuta unanitania
Maana moyo wangu nimekupa uweke
Mimi ni mfungwa tena ni mjinga

Nimejileta gerezani
Tena sikuwaza ntakuwa mateka
Mmh

Najua ulinizungusha sana
Sijali huwa ni mambo ya ujana
Kukupenda wewe sijuti

Maneno yalisemwa mengi sana
Kuna wakati nilikata tamaa
Kukupenda wewe sichoki

(Moyo mashine) ila majibu ya upendo ulishakosa
(Acha waseme) nimekupendea nini
(Moyo mashine) ila majibu ya upendo ulishakosaga

(Wacha waseme) nimekupendea nini
Nafsi inanituma upendo uko nje ya maneno
Ila vitendo

Kama bubu akipenda atanena vipi kwa maneno
Pasina vitendo?
Kiziwi, hata ukimwambia “nakupenda” wala hasikii

Ila vitendo oh
Wewe sijui sababu za kukupenda
Siwezi sema, ila utaona ah

Najua ulinizungusha sana
Sijali huwa ni mambo ya ujana
Kukupenda wewe sijuti

Maneno yalisemwa mengi sana
Kuna wakati nilikata tamaa
Kukupenda wewe sichoki

(Moyo mashine) ila majibu ya upendo ulishakosa
(Acha waseme) nimekupendea nini
(Moyo mashine) ila majibu ya upendo ulishakosaga

(Wacha waseme) nimekupendea nini
Oh kama moyo ulisimama nlipokuona
Hukuongea, hukucheka, nilikuona tu

Na tabia sikufahamu, labda niache mwanadamu
Ukipenda usishangae ni upofu wa moyo
Kumbe moyo ulinirubuni, hukusema umependa nini

(Moyo mashine) ila majibu ya upendo ulishakosa
(Acha waseme) nimekupendea nini
(Moyo mashine) ila majibu ya upendo ulishakosaga

(Wacha waseme) nimekupendea nini